Skip to main content

NABII DAR ADAI SHETANI AMEFARIKI TANGU NOVEMBA 4, 2008.







.
Mtume  na  Nabii  Nduminamfoo  Munuo.



HUKU  akiwa  na  matawi  karibu  nchi  nzima, na  kanisa  lake  likiwa  linakua  kwa  kasi, Mtume  na  Nabii  Nduminamfoo  Munuo, wa  kanisa  la  Siloam  ( Shika  Neno  Tenda  Neno ), ambaye  awali  alianza  kujiita  Nabii  Eliya, hivi  sasa  amejiongezea  jina  jingine  akijiita  Mungu  wa  Majeshi.

Kwa  mujibu  wa  jarida  liitwalo    Neema Kubwa”  lililotolea  na  gazeti  hili  hivi  karibuni, Mtume  na  Nabii  Munuo  pia  anajiita  AD2, akidai  yeye ndiye  roho  ya  Adamu  wa  Pili, ambayo  huleta  uzima  kinyume  na  ya  Adamu   wa  kwanza  iliyoleta  mauti.

Jengo  kuu  la  ibada  la  kanisa  hilo  liko  maeneo  ya  Makonde  Mbezi  Beach.
Biblia  katika  1 Wakorintho 15:45  inasema    Ndivyo  ilivyo  andikwa, Mtu  wa  kwanza, Adamu  akawa  nafsi  iliyo  hain;  Adamu  wa mwisho ni  roho  yenye  kuhuisha “.
Mmoja wa  waumini  wake  anayesimamia  jarida  hilo, alisema  hakuna  cha  kushangaza  kwa  nabii  huyo  kuitwa  Mungu  wa  Majeshi  kwa  kuwa  ni  jina  alilolichagua  mwenyewe  kwa  ufunuo  maalumu.

Munuo, ambaye  anaamini  kuwa  huduma  yake   itaenea  dunia  nzima, kwa  vile  ndani  yake  ipo  roho  ya  Eliya, jina  linalo  maanisha “ Mungu  Mwokozi “  amewaaminisha  wafuasi  wake  kuwa siku  moja  dunia  nzima  itaongozwa  kidini  na  yeye  na  viongozi  wengine  wote  wa  kidini  watamwelewa  taratibu.

Baadhi  ya  mambo  tata  ya  kiimani  ambayo  nabii  Munuo  amewasadikisha   maelfu  ya  waumini  wake  ni  pamoja  na  kwamba  mafunuo  yake  ni  makamilifu  na  hairuhusiwi  kuyahoji  wala  kuyapima  na  Biblia.


Sambamba  na  hilo, waumini    hao ambao  pamoja  na  kiongozi  wao , wote  huvaa  mavazi  meupe  wawapo  ibadani   hawakubali  kwa  namna  yoyote  kutumia    Biblia  yenye  jalada  jeusi, na  badala  yake  huyachana  na  kuweka  ya  kwao  meupe  ambayo  ni  rangi  ya  nuru.


Ingawa  waumini  wa    Siloam  wanaamini  kwamba, mtu  anaweza  kuandamwa  na  mapepo  kutokana  na  sababu  mbalimbali  ikiwa  ni  pamoja   na  kuwa  na  majina  yenye mafungamano  na  mizimu, wanaamini  kuwa  Shetani alifariki  Novemba  4, mwaka  2008.


Kwa  mujibu  wa   mafundisho  ya  kanisa  hilo, Bustani  ya  Edeni  inayo  tajwa  katika  Biblia  ilikuwa  Tanzania, na  ndiko Adamu  na  mkewe  walikoishi  ndiyo  maana  kuna  amani  kuliko  mataifa  mengi  duniani.
Mmoja  wa  waumini  wake  aliye  bobea   katika  mafundisho  ya  kanisa  hilo, ambaye  pia ni  Mhariri, Bi.  Scolastica  Msewa, alimwambia  mwandishi  wetu  kuwa  wanadamu   wote  duniani  asili  yao  ni  Tanzania, na  ndiyo  maana  mwanamke   wa  Kiafrika  anaweza  kuzaa  mtoto   wa  rangi  yoyote  duniani  wakati  jamii  za  weupe  hawawezi  kuzaa  mwafrika.    Mungu  alikoanzia  ni  lazima  amalizie hapo hapo”’ alisema.
Waumini  wa  kanisa  hilo  pia  hutakiwa  kubadilisha  majina  yao  ya  ukoo  kwa  kuwa  mengi  ya  majina  hayo  yanabeba  laana.
Zaidi  ya  hapo  kwa  mujibu  wa  uchunguzi  wa  gazeti  hili, muumini  huunganishwa  katika  familia  nyingine  hapo  kanisani  na  hutengwa  na  wazazi  na  ndugu  wa  kimwili.

Wakati  wa  maombi  ni  lazima  muumini  ajiunganishe   na  madhabahu  kuu  ya  Nabii  Munuo  (  Eliya  Mungu  wa  Majeshi  AD 2 )  ili  yaweze  kusikilizwa.
Kituko  kingine  cha  wana   Siloam, ni  kwamba  wakati  wanapo mwombea  mgonjwa  mwenye  mapepo  au  mizimu  huyahamishia  hayo  mapepo  kwa  mmoja  wao  kisha  wanaanza  kukemea  na  huyo  mmoja  wao  baada  ya  kupagawa  hayo  mapepo  huongea  kupitia  kwake.
CHANZO  : Gazeti  La  Nyakati, Toleo Na. 696, tarehe  30  Machi 2014.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA