Skip to main content

BAJETI YA HARUSI YA GHARAMA NDOGO






Gharama  za  sherehe  ya  harusi  ni  jambo  linalo  waumiza  maharusi  wengi  wanao  tarajia  kufunga  ndoa .
Hata  hivyo,  maharusi  na  familia za  maharusi  wakiamua  kiweka  mambo  ya  kuonyesha  ufahari  pembeni,  wanaweza  kufanya  sherehe  ya  harusi  kwa  gharama  ndogo  sana.

So far  mpaka  sasa, harusi  iliyo  ripotiwa  kufanyika  kwa  gharama  ndogo  kuliko  zote  nchini  Tanzania  ni  iliyo  fungwa   na  wanandoa   Bw. Charles  Kanyema  ( 29 )  na  Bi. Honoratha  Paschal  (  28  ).
Sherehe  ya  ndoa  hiyo  iliyofungwa  katika  Parokia  ya  Morogoro  mjini, mnamo   mwezi  Juni  mwaka  2013  iligharimu  kiasi  cha  Shilingi  Elfu  Arobaini  na  Tano  tu  za n kitanzania ( Tshs.45,000/=).  Kwa  habari  zaidi  kuhusu   wanandoa  hawa  unaweza  kutembelea  link  hii  hapa   chini; http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/waenda-kufunga-ndoa-kwa-bodaboda-warudi-kwa-miguu
Katika  mada  iliyo  jadiliwa  kwenye  mtandao  mmoja  wa  kijamii  nchini  kuhusu   gharama  za  kufanya  harusi  kwa  bei  nafuu, maoni  mbalimbali  yalitolewa  na  watu  mbalimbali.
Yafuatayo  ni  baadhi  ya  maoni  hayo, na  ambayo  naamini  yanaweza  kuwa  msaada  kwa  maharusi  wanao  jiandaa  kufunga  ndoa  hivi  karibuni.

Shilingi  Milioni  Tano, inatosha kufanya harusi kubwa sana ya watu 120 hadi 150. Kuna harusi ilifanyika 22.02.2014 jamaa walitumia 9.2million harusi ya watu around 300 ilikua bomba balaa. tulikunywa na kula nyama mwanzo mwisho na kamati yao ikatoa zawadi fedha taslim 1.270m kama zawadi. Mimi mwenyewe nilikua impressed sana maana nategemea kufunga ndoa mwaka huu na niliambiwa ukionanan na wenye ukumbi wanaweza kukupangia kila kitu. Ukumbi wenyewe Princess hall Sinza.

Mtoa  maoni  mwingine  alisema    :

Katika harusi yangu nilifanya hivi, nilifanya 201O ilikua hivi

1.Budget haikuzidi milioni 4, nyingi zilienda kwenye chakula
2.Sikutoa kadi hata moja ya mchango
2. niliamua iwe casual, kwa hiyo sikuhangaika kutauta profesional MCs, badala ya kuchangisha afu kumlipa MC, tulitengeneza ratiba kisha marafiki zangu wachache, wakasaidia kusema chochote kwa kupokezana.
3. Badala ya kuchanga pesa kukodi magari, tulitumia magari ya friends, niliomba rafiki zangu wengine wachukue maids, mwingine bibi harusi, mwingine mama mkwe..kwa gari zetu hizi hizi za kawaida
.

Mtoa  maoni  mwingine  aliingia  ndani  zaidi  na  kutoa  mchanganuo  wa  gharama  za  sherehe  ya  harusi.   Alitoa  mawazo  yafuatayo :

1.Ukumbi=1,000,000

2.Mapambo=1,000,000

3.Vinywaji bia 3@=330,000

4.Chakula plate 12000=600,000

5.Mc & Music=600,000

6.Magari-
Wazazi pande zote mbili=300,000

7.Gari-Maharusi=400,000

8.Coaster(Waalikwa)=
150,000.

Daaah nlisahau hela ya keki, sasa tusiivuruge hela ya dharura; twende tuvunje pale kwenye gari ya Maharusi, chanja 200,000 hapo afu tuitupie kwenye cake, ibaki 200,000 Gari safi na simple

Jumla kuu  =4,380,000
Balance=620,000(Dharura)


Mtoa  maoni  mwingine  alitoa  mchanganuo  wa  harusi   yake, ambayo  aliifanya  kwa  gharama   ya  kawaida.

Natoa mchanganuo wa harusi tuliyofanya sisi. Ukumbi 600,000 unawekewa viti vya plastics na kupambiwa (750,000 unapata executive chairs) sisi tuliweka viti vya plastics (600,000) mapambo tulipamba simple standard kwa (600,000), usafiri wakwe tuliwapa hela 150,000 watafute usafiri wao wenyewe maharusi 300,000 wazazi 130,000, keki ndafu moja 200,000, Champaign 6 (72,000), MC na music 500,000, Picha 750,000, chakula cha watu 160 (ng'ombe mkubwa 560,00, kuku 20 kwa 100,000, kuchoma nyama kupika wali mweupe na pilau na ndizi za kuchemsha 780,000) vinywaji (1,934,00) jumla ilikua 6,800,000

Na  mwingine, akaelezea  kuhusu  bajeti  ya  wedding reception  yake  kama  ifuatavyo :

Budget ya my wedding reception was around 2million, it was a simple one ilifanyika nemax royal hotel, kinondoni. Waalikwa walikuwa 60. Kulikuwa hakuna kamati wala sikumchangisha mtu hata senti

Mgawanyo wa budget:
1. chakula 20,000@plate X 60=1.2m
2.vinywaji 3 beers/person @ 2500X60=450000
3.mapambo bi harusi=100,000
4.gari ya wakwe=60,000(from a good friend).
5.cake=100,000
6. still pictures=150,000
7. champaignes(non alcoholic)2@9000=18000
Total 2.078m.
note; mc alikuwa one of my sisters, mziki pale ukumbini kulikuwa na speakers, so tulikuja na laptop yetu my bro akawa dj. Pia hatukulipia gharama za ukumbi maana tulielewana na wenye ukumbi coz vinywaji na chakula tulichukua pale pale. Pia hatukuwa na gharama za kupamba ukumbi;ila walituwekea nice chairs and tables zilizopambwa na vitambaa gari tuliyotumia maharusi ilikuwa a friend's car

Ni  matumaini  yangu  kuwa, makala  yatawasaidia  maharusi  ambao  wanajiandaa  kufunga  ndoa  hivi  karibuni  na  wanafikiria  kufanya  sherehe  ya  harusi  kwa  gharama   ndogo.
MUNGU  AWABARIKI  SANA  NA  NINAWATAKIA   MAANDALIZI MEMA.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA