Skip to main content

JINSI YA KUZUIA AU KUPUNGUZA MAGONJWA SUGU YASIYO YA KUAMBUKIZA

Mlo  Kamili

Magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yanaweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kufuata mtindo bora wa maisha. Mtindo bora wa maisha ni muhimu katika kuendeleza na kudumisha afya ya mtu na kuzuia maradhi, hususani magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia ulaji unaofaa, kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, kuepuka matumizi ya pombe, na kuepuka msongo wa mawazo.

Ulaji unaofaa:

Ulaji unaofaa hutokana na kula chakula chenye mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi matano ya vyakula na kupunguza kiasi cha mafuta, chumvi, na sukari kinachotumika.
Ulaji unaofaa unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri, mzunguko wa maisha (mfano utoto, ujana, uzee), hali ya kifiziolojia (mfano ujauzito, kunyonyesha), kazi au shughuli na hali ya afya.
Ulaji unaofaa huchangia katika kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza maradhi, yakiwemo magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.

Mambo ya kuzingatia ili kufanikisha ulaji unaofaa:

• Kula mlo kamili mara tatu kwa siku.
• Kula matunda na mboga mboga kwa wingi kila siku.
• Kula vyakula venye makapi mlo kwa wingi.
• Epuka kutumia sukari nyingi.
• Epuka kula vyakula venye chumvi nyingi.
• Kunywa maji safi, salama na ya kutosha
• Kula asusa zilizo bora kilishe.
Kufanya mazoezi ya mwili :
Ni muhimu kwa binadamu wote, mtoto au mtu mzima, mnene au mwembamba, mgonjwa au mwenye afya njema kufanya mazoezi kwani husaidia mifumo mbalimbali ya mwili kufanya kazi kwa ufanisi. Mazoezi hupunguza uwezekano wa kupata saratani, ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo, na shinikizo kubwa la damu.
Mazoezi husaidia pia katika kuzuia ongezeko la uzito wa mwili, kupunguza msongo wa mawazo, na pia huboresha afya ya akili ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo wa kufikiri, kuelewa na kukumbuka. Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili angalau kwa dakika 30 kila siku, yaani mazoezi yanayotumia nguvu kiasi kama kutembea kwa haraka.
Anza kwa kutembea kwa muda mfupi, na baadaye unaweza kuongeza muda hadi dakika 60 kila siku, ukishindwa kabisa kufanya kila siku fanya angalau dakika 60 mara tatu kwa wiki.
kuepuka matumizi ya pombe:

Pombe husababisha ongezeko la uzito wa mwili ambalo linahusishwa na magonjwa mengi sugu yasiyo ya kuambukiza. Tafiti zimethibitisha kwamba pombe inaongeza sana uwezekano wa kupata saratani hasa ya mdomo, koo, koromeo, matiti, utumbo mpana na ini.
Tafiti zimeonyesha kwamba pombe ina madhara mengikiafya, ikiwa ni pamoja na kusababisha magonjwa, kupunguza uwezekano wa ini kufanya kazi vizuri, na pia huathiri uwekaji wa virutubishi mwilini.
Endapo unakunywa pombe kwa mwanaume inashauriwa kunywa vipimo viwili ambavyo ni sawa na milimita 500 za bia, mvinyo milimita 200, na pombe kali milimita 50 kwa siku . Kwa mwanamke anashauriwa kunywa nusu ya vipimo vinavyotumika kwa mwanaume.

Kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku:

Uvutaji wa sigara, utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo, saratani ( hasa za mapafu, kinywa na koo), magunjwa sugu mengine ya njia ya hewa, shinikizo kubwa la damu na vidonda vya tumbo hivyo ni muhimu kuepuka.
Sumu aina ya nikotini iliyopo katika sigara huharibu ngozi ya ndani hivyo huongeza uwezekano wa lehemu kujikusanya kwenye sehemu za mishipa ya damu zilizoathiriwa. 21
Nikotini pia huweza kusababisha mishipa ya damu kuziba au kuwa myembamba kuliko kawaida na hivyo kuzuia damu kupita inavyotakiwa . Matumizi ya sigara pia huweza kuleta athari kwa wale walio karibu na mvutaji hususani kwa mama mjamzito na mtoto.

Kuepuka msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo ni hisia ambayo huweza kuamshwa na matukio mbali mbali kama vile kufiwa na mtu wa karibu, kukabiliwa na tatizo katika( familia,maisha au shuleni), kuwa na kazi nyingi kwa muda mrefu bila ya kuwa na muda wa kupumzika. Hisia hizo zinaweza kusababisha hasira, wasiwasi, woga, huzuni, kuchanganyikiwa na pia kukata tamaa. Msongo wa mawazo ukijitokeza mara kwa mara huweza kusababisha ulaji usiofaa na mifumo ya mwili kutofanya kazi vizuri
Inashauriwa kupunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi, kujipa muda wa kupumzika, kushiriki katika shughuli mbali mbali kama michezo, matamasha, harusi, na pia kupangilia vizuri jinsi ya kutumia muda wako. Jadili na mtu unayemwmini kuhusu matatizo yako, cheka au angua kilio, zima simu yako kwa muda katika siku.

HITIMISHO
Watu wengi tunakumbwa na magonjwa haya kutokana na kuwa na mtindo wa maisha usiofaa, ni vyema kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
USHAURI
 Ni vyema kushiriki katika michezo, na mazoezi ya viungo.
 Ni muhimu kujenga mazoea ya kupima mara kwa mara afya zetu.
 Tuzingatie mtindo bora wa maisha ili kuzuia au kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza. 

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA