Skip to main content

FAIDA ZA KIAFYA ZA MAFUTA YA NAZI


Mafuta  ya  nazi  yana  faida  nyingi  kwa  mwanadamu. Ni  kusudio  langu  kushare  na  wewe  msomaji  wangu  taarifa  kuhusu  faida  mbalimbali  zitokanazo  na  mafuta  ya  nazi. Fuatana  name  hadi  mwisho  wa  makala  haya. Kutokana  na  urefu  wa  makala  haya, nitayagawa  katika  sehemu  ya  kwanza  na  ya  pili na  kama  sehemu  mbili  hazitatosha  basi  nitaongeza  na  sehemu  ya  tatu.
Mafuta  ya  nazi  yamekuwa  yakitumika  kama  chakula  na/au   urembo  kwa  maelfu  ya  miaka. Mafuta  ya  nazi   yana  uwezo  mkubwa  sana  wa   kuharibu aina  zote  za  vijidudu, virusi  na  bacteria   hatari  kwa  ustawi  wa  afya  ya  mwanadamu  . Mafuta  haya  huupatia  mwili  wa  mwanadamu  mafuta  ambayo  ni  muhimu  kwa  afya  ya mwanadamu.
Karibu  asilimia  hamsini  ya  mafuta  ya  nazi  ni  lauric  acid ambayo  ni vigumu  sana  kupatikana  au  haipatikani  kabisa. Kwa ufupi  mafuta  ya  nazi  yana  kiwango kikubwa  cha  lauric  acid kuliko  kitu chochote  kile  hapa duniani.
Mwili  wa  mwanadamu   hubadili  lauric  acid kuwa  monolaurin. Monolaurin  ni  aina  ya  monoglyceride  ambayo ina  uwezo  mkubwa  sana  wa  kupambana  na    nguvu  ya  virusi, na  bacteria  kama vile  giardia  lamblia.
Matumizi  ya  mafuta  ya  nazi  eidha  kama  chakula  ama  kama  urembo  yana  faida  kubwa  sana  za  kiafya  katika  mwili  wa  mwanadamu.
Mafuta  ya  nazi  husagika  kwa  urahisi  katika  mfumo  wa  usagaji  chakula  wa  mwanadamu na   hayana  madhara.    Mafuta  haya  hayatengenezi  sumu  kwenye  mkondo wa  damu, hivyo  basi   ili  kupata  ama  kuongeza  nishati  ya  kutosha   kwenye  mwili  wako, unashauriwa   kula  walau  vijiko  viwili  vya  mafuta  ya  nazi  kwa  siku  au kula  chakula  kilicho  ungwa  kwa mafuta  ya  nazi  kama  vile  wali  au  maharage.

Mafuta  ya  nazi   yanafaa  kwa  aina  zote  za  mapishi kwa  sababu  yana uwezo  wa  kustahimili  joto  bila  kuharibika  kama  ambavyo  aina  nyingine  za  mafuta  zinavyo weza  kuharibika  kutokana  na  joto  kubwa  mfano  mafuta  ya  mzeituni.
Kama  hiyo  haitoshi, mafuta  ya  nazi  huwa  hayawezi  kuchacha  kama  aina  zingine  za  mafuta ,jambo  ambalo  ni  faida  kubwa  sana  kwa  watu  walio  wekeza  kwenye  biashara  ya  utengenezaji  wa  mafuta  ya  nazi.

FAIDA  ZA  JUMLA  ZA  MAFUTA  YA  NAZI
1.             Mafuta  ya  nazi  huimarisha  afya  ya  moyo wa  mwanadamu.
2.          Mafuta  ya  nazi huimarisha   afya  ya  ubongo  wa mwanadamu  na  kusaidia katika  kuufanya  ubongo  wa  mwanadamu  kuwa  na  ufanisi  thabiti.
3.           Mafuta  ya  nazi  yanasaidia  kuuimarisha  mfumo  wa  mmen’genyo wa  chakula  katika  mwili  wa  mwanadamu  na  hivyo  kusaidia  katika  kupunguza  uzito  au  kumuepusha  mwanadamu  na  kuwa  na  uzito  mubwa.
4.          Mafuta  ya  nazi  yanaimarisha   mfumo  wa  kinga  ya  mwili  wa  mwanadamu.
5.           Matumizi  ya  mara  kwa  mara  ya  mafuta  ya  nazi  husaidia  katika  kuifanya  ngozi  ya  mwanadamu  kuwa  yenye  afya  njema  na  kumfanya  muhusika  kuonekana  kijana.

Katika  makala  yanayo  fuata, tuatelezea  faida  nyinginezo  za  matumizi  ya mafuta  ya  nazi.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA