Total Pageviews

Wednesday, April 16, 2014

HII NDIO NYUMBA PEKEE YA MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU ZAKARIA KAKOBE.


Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. 


Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.


Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao. 


Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.


Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".


Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. 


Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.


Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.


CHANZO : JAMII  FORUMS

Monday, April 14, 2014

SABABU KUMI NA NANE ( 18 ) KWA NINI UNATAKIWA KUPUNGUZA UZITO.Unene  ni tatizo  linalo  wakabili  watu  wengi  duniani. Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, unene  una  madhara  makubwa  kuliko  inavyo  dhaniwa.
Hizi  ni  sababu  18  kwa  nini  unatakiwa  kupunguza  unene.

1.    Unene  unaongeza  kiwango  cha  mafuta  mwilini, ambayo  huongeza  uwezekano  wa  kupata  kansa.

2.  Unene  unaongeza  mafuta  mwilini, ambayo  hufanya  matibabu  ya  kansa  kuwa  magumu  zaidi.

3.  Unene  huongeza mafuta  mwilini  ambayo  hushinikiza  na  kuubana  moyo.

4.  Mtu mnene  huwa  mvivu  kufanya  mazoezi, suala  ambalo  humuongezea  zaidi  unene.

5.  Mafuta  mengi  mwilini  yana  madhara  kwa ubongo.

6.  Unene  huongeza  uzito  katika  mifupa  na  viunga  vya  mifupa  ( bone  joints )

7.  Unene  husababisha kibofu  cha  mkojo  kibanwe  suala  linalo  sababisha  matatizo   mbalimbali  ya  mkojo.

8.  Unene  hupunguza  uwezo  wa  kujamiiana  wa  mtu.

9.  Unene   hupunguza  uwezo  wa  kuzaa  na  hata  kusababisha  utasa  na  ugumba.

10.               Unene  husababisha kibofu  cha  mkojo  kibanwe, suala  linalo  sababisha  matatizo  mbalimbali  ya  mkojo.

11. Unene huweza  kuufanya  mwili  upatwe  kwa  wepesi  na magonjwa  mbalimbali  kama  vile  kisukari  na  presha.

12.               Watu  wanene  wanapofika  hospitalini, upimaji  wao  pia  huwa  wa  matatizo.

13.               Unene  husababisha  ujauzito  kuwa  wenye  matatizo  mengi.

14.               Unene  huathiri  pia  afya  ya  motto  mchanga  anaye  zaliwa.

15.               Unene  hufanya  matibabu  ya  pumu  ( asthma ) yawe  magumu.

16.               Unene  hupelekea  mtu asilale  vizuri  na  wakati mwingine  mtu  mnene  anapolala  hubanwa na  pumzi  suala  linalo mfanya   aamke  mara  kwa  mara.

17.               Unene  humfanya  mtu  ashindwe  kuwajibika vizuri  kazini  na  hata  kuathiri  utendaji  kazi  wake.

18.               Unene  hufanya  matumizi  ya  fedha  kuwa  makubwa   unapokumbwa  na  magonjwa  yasababishwayo  na  unene.

Friday, April 11, 2014

Walimu wanahitajika kwa haraka sana

Walimu wa masomo yafuatayo wanaitajika kwa haraka sana. Civics , History , Geography,Kiswahili, Mathematics, Physics na Chemistry .Kituo cha kazi kipo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera . Shule inatoa huduma ya chakula,usafiri na makazi kwa walimu wanaoishi nje ya shule. Kwa mawasiliano piga 0757297942 au 0787974003 karibu sana.
SOURCE : JAMII  FORUMS.

Kitabu; Richard Branson–Mafunzo Ya Maisha(Screw It, Let's Do It)
  Mwezi huu tutajisomea kitabu kilichoandikwa na Richard Branson kinachoitwa SREW IT, LETS DO IT, LESSONS IN LIFE.
Richard Branson ni bilionea wa kiingereza ambaye utajiri wake unakadiriwa kufikia dola bilioni 5. Richard ni mwanzilishi na mwendeshaji mkuu wa kundi la makampuni lijulikanalo kama Virgin Group. Katika kundi hili anamiliki makampuni zaidi ya 400. Ni kitu cha kipekee sana kwa mtu mmoja kuweza kuendesha makampuni 400 yenye wafanyakazi zaidi ya 16,000.

Richard Branson alianza ujasiriamali akiwa na miaka 16 baada ya kuacha shule. Kilichomfanya aache shule ni kutokana na tatizo la kushindwa kuelewa, yani alikuwa mzito sana kuelewa darasani. Anasema mwalimu mkuu wa shule yake alimwambia atakuwa bilionea au ataishia jela.
Baada ya kuacha shule Richard alianzisha jarida lake ambalo alikuwa akiandika mambo yanayohusu wanafunzi. Baadae alifungua studio ya kurekodi muziki na biashara zake zikaendelea kukua mpaka kufikia makampuni zaidi ya 400.
Katika kitabu hiki Screw It, Lets Do It, Richard anaelezea misingi aliyosimamia kwenye maisha yake na ikamuwezesha kufikia mafanikio makubwa aliyonayo sasa. Misingi hiyo sio siri kubwa sana bali ni mambo ya kawaida ambayo hata mimi na wewe tunaweza kuyafanya na tukafikia mafanikio makubwa.
Moja ya misingi aliyosimamia ni; Kufanya tu(Just Do It). Katika kufanya tu, Richard anakushauri yafuatayo;
1. Amini kwamba inawezekana
2. Kuwa na malengo
3. Ishi maisha yako
4. Usikate tamaa
5. Jiandae vizuri
6. Jiamini
7. Wasaidie na wengine.
Misingi mingine anayotufundisha Richard ni;
Kuwa na furaha, Jipe changamoto, Simama kwa miguu yako, Ishi wakati huu, Thamini familia na marafiki, Kuwa na heshima, Fanya mambo mazuri.
Kitabu hiki ni kifupi sana na unaweza kukisoma na kukimaliza ndani ya masaa mawili. Ni kitabu ambacho kitakupa mafunzo makubwa sana kuhusu maisha na mafanikio.
Nakusihi sana ukisome kitabu hiki kwani kitakuwa na msaada mkubwa kwako. Hata kama hujawahi kusoma kitabu kingine chochote nilichowahi kutuma, tafadhali sana soma kitabu hiki tu. Kitakufungua na kukuonesha kwamba hakuna lisilowezekana.
Kitabu hiki kimetumwa kwa wanachama wa mtandao wa AMKA MTANZANIA. Kama hujakipata kitabu hiki bonyeza maandishi haya na uweke email yako kisha utatumiwa email yenye link ya kitabu papo hapo, ni bure kabisa.
Nakutakia kila la kheri katika harakati zako za mafanikio.
Kumbuka Tuko Pamoja.

CREDIT :  AMKA TANZANIA  BLOG